Members wa familia hiyo wameendelea kile alichokifanya dada yao, Kim Kardashian aliyempokonya Amber Rose rapper Kanye West, ambapo hivi karibuni mdogo mtu Khole Kardashian ameripotiwa kuanza uhusiano wa karibu na staa wa NBA, James Harden ambaye aliwahi kuwa na uhusiano na Amber Rose.

Februari mwaka huu, Amber alikaririwa akielezea uhusiano wake na mcheza kikapu huyo, “mimi na James tuna urafiki ‘special sana’ kwa kweli.” Huenda kauli hiyo iliyagusa masikio ya the Kardashians ambao wana bifu la wazi na Amber Rose hivyo wakaamua kujisogeza kwenye chimbo lake jipya.

Chanzo cha karibu na Amber Rose kimeeleza kuwa mwanamitindo huyo amekasirishwa na kitendo hicho anachokitafsiri kama kuamua kumuingilia kila anapopita.

Bifu la wazi kati yao lilianza baada ya Amber Rose kueleza kumchana Kim Kardashian kwenye mahojiano na kituo kimoja cha radio akidai kuwa ni ‘fake’, lakini pia aliuponda kitendo cha Tyga kuanzisha uhusiano na mdogo wake Kim Kardashian, Kylie Jenner mwenye umri wa miaka 17.
Amberr
Bifu hilo lilihamia kwenye mitandao ya kijamii na kutengeneza timu zilizorushiana maneno makali.
Watu wa karibu wa Amber Rose wanahofia huenda mmoja kati ya wanafamilia hao wa Kardashians wakaamua kumnyemelea Wiz Khalifa pia.

“Hao Kardashians wana kiu kweli. Amber hatashangaa kama mmoja kati yao atajisogeza tena kwa Wiz Khalifa,” alisema mndani wa Amber Rose. Japo kuliwahi pia kuzuka tetesi kuwa Khole aliwahi kuwa karibu na Wiz Khalifa.

Keko Wa Uganda Atimuliwa Coke Studio Baada Ya Kuvuruga
West Ham Wamnyemelea Zaidi ‘Mnigeria’ Wa Juventus