Wadau wa soka la Bongo Philemin Ntahilaija na Swed Mkwabi (mwenyekiti wa zamani wa Simba) leo June 8, wamejitokeza hadharani na kumchukulia fomu Rais wa TFF anaetetea nafasi yake Wallace Karia.

Wadau hao walifika kwenye ofisi za TFF na kufuata utaratibu wa kumchukulia fomu za kuwania nafasi ya Urais Karia.

Baada ya kukamilisha zoezi hilo ndani ya ofisi za TFF, walitoka nje na kutoa uthibitisho wa fomu pamoja na risiti za malipo mbele ya waandishi wa habari.

Uchaguzi mkuu wa TFF umepangwa kufanyika jijini Tanga mwezi Agosti mwaka huu, huku kamati ya Uchaguzi ikitoa wito kwa wadau wa soka kujitokeza kwa wingi ili kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Shirikisho hilo.

Tarimba Abbas: Wengi wananishawishi kugombea Urais TFF
Maoni ya Manara usajili wa Bongo