Mchambuzi wa Soka la Bongo kupitia kituo cha Radio cha EFM Oscar Oscar, amechukua fomu za kuwania nafasi ya Urais wa Shirikisho la soka nchini TFF, ikiwa ni haki yake kwa mujibu wa katiba ya Shirikisho hilo.

Oscar ambaye mara nyingi amekua mkosoaji wa baadhi ya mambo ya soka la Bongo, alifika ofisi za TFF leo Jumatano (Juni 09), akiwa na mtangazaji wa kituo cha EFM Tunu Shenkome na mchambuzi mwenzake Gef Lea.

Baada ya kukamilisha zoezi la kuchukua fomu, Oscar alithibitisha kupatiwa fomu hizo za kuwania kito cha Urais kwa kupiga picha na kisha kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Hatua ya Mchambuzi huyo kuchukua fomu za kuwania nafasi ya kiti cha Urais, ni dhahir atapambana na Rais aliyetangaza kutetea nafasi yake Wallace Karia, ambaye jana Jumanne (Juni 08) alichukuliwa fomu na wadau wa soka Swed Mkwabi na Philemin Ntahilaija.

Wakati huo huo Mjumbe wa kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka nchini TFF  Lameck Nyambaya naye amechukua fomu za kuwania nafasi hiyo kwa mara nyingine.

Lameck Nyambaya (kushoto) akiwa na mwandishi wa habari za michezo wa kituo cha Clouds FC Shaffih Dauda

Lameck ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Soka Mkoa Wa Dar es salaam (DRFA), alifika ofisi za TFF akiwa na mwandishi wa habari za michezo wa kituo cha Clouds FC Shaffih Dauda.

Uchaguzi mkuu wa TFF umepangwa kufanyika jijini Tanga mwezi Agosti mwaka huu, huku kamati ya Uchaguzi ikitoa wito kwa wadau wa soka kujitokeza kwa wingi, kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Shirikisho hilo.

Museveni ateua Makamu wa Rais mwanamke
Rais wa Botswana kufanya ziara Tanzania