Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia  amepokea kwa masikitiko na majonzi makubwa taarifa za kifo cha Mbunge wa Songea Mjini (CCM), Leonidas Gama.

Kutokana na msiba huo, Rais Karia ametua salamu za rambirambi kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Kadhalika Rais Karia ametuma salamu za salamu rambirambi kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Ruvuma (FARU), Golden Sanga pamoja na Mwenyekiti wa Majimaji ya Songea, Steven Ngonyani na wanafamilia wote wa mpira wa miguu na wananchi wote wa mjini Songea.

“Songea ina historia ya mpira na akina Gama ni chachu ya maendeleo ya mpira wa miguu Songea. Tumepoteza hazina nyingine, lakini niombe tu familia ya Gama, ndugu, jamaa na marafiki kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu kwao,” amesema.

“Nawapa pole nyingi sana na kupitia viongozi wa FARU, Majimaji, Mlale JKT na wanafamilia wengine wa soka katika Mkoa wa Ruvuma, naomba mfikishe salamu zangu za pole kwa familia ya marehemu,” amesema Rais Karia.

Rais Karia amesema anamkumbuka Gama kwa uhodari wake katika nyadhifa mbalimbali za uongozi ikiwemo ukuu wa wilaya, mkoa na ubunge kwani alifanya kazi kwa kujiamini na kupenda kupigania maendeleo hususani mpira wa miguu bila kuchoka.

Uamuzi wa kamati kuhusu usajili ligi ya wanawake
Maafande wa magereza waikomaliza Young Africans