Klabu ya Arsenal inaendelea kuhusishwa na Mshambuliaji mpya katika dirisha la usajili la Januari, ukiacha na Ivan Toney na sasa Karim Benzema, ni jina kwenye midomo ya kila mtu kuwa anatua ‘The Gunners’.

Mbali na hivyo, huku kwingine hapo hapo Arsenal mustakabali wa Emile Smith Rowe ukionekana kutokuwa na uhakika.

Arsenal ilionyesha bado hawajaondoka kwenye mbio za ubingwa kwa ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya Crystal Palace wikiendi iliyopita na kujibu maswali ya kama wamo kwenye mbio za ubingwa au hawapo.

Mustakabali usio na uhakika wa Karim Benzema nchini Saudi Arabia umesababisha uvumi kuwa mshindi huyo wa Ballon d’or 2022 anaweza kupatikana mwezi huu.

Mbali na Arsenal, pia Chelsea wamekuwa wakihusishwa na Mshambuliaji huyo kutoka nchini Ufaransa, ambaye hivi karibuni aliweka mgomo wa kurejea klabuni kwake akisisitiza timu hiyo inunue wachezaji wanaoweza kupambana.

Makala: Mkongwe Caligula na cheko la kujitekenya
Trezeguet: Misri itawashangaza wengi AFCON 2023