Mahambuliaji kutoka nchini Ufaransa Karim Mostafa Benzema leo amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu bingwa barani Ulaya Real Madrid.

Benzema amesaini mkataba wa miaka minne, ambao utamuwezesha kulipwa mshahara wa Pauni milioni 890 kwa kipindi chote, hadi mwaka 2021.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29, amekamilisha mpango huo baada ya mazungumzo ya muda mrefu kati yake na uongozi wa Real Madrid ambao ulionyesha kuhitaji huduma yake kwa kipindi kingine kijacho.

Makubaliano hayo ya mkataba mpya, yanamuwezesha Benzema kuwa sehemu ya wachezaji watakaokaa klabuni hapo kwa kipindi kirefu, miongoni mwa wachezjai waliopo kikosini kwa sasa, na inaaminiwa bado uwezo wake utaendelea kuleta mafanikio chini ya utawala wa meneja Zinedine Zidane.

Mpaka sasa Benzema ameshaitumikia Real Madrid katika michezo 371 na kufunga mabao 181.

Benzema ambaye tayari ameshaitumikia timu ya taifa ya Ufaransa katika michezo 81, alijiunga na Real Madrid mwaka 2009 akitokea Olympic Lyon kwa ada ya Pauni milioni 41.

Ibrahim Akilimali ashtukia mgomo wa wachezaji
Q Boy awafungukia wanaosema hajui kuimba