Aliyekuwa mgombea mwenza wa Raila Odinga, katika Uchaguzi Mkuu wa Agosti, 2022 nchini Kenya, Martha Karua amesema hatua ya Baraza la mawaziri la Uhuru Kenyatta, kuidhinisha GMO na Rais William Ruto haikuwa halali na ilikuwa ni kinyume cha sheria.
Karua, ambaye pia ni Bosi wa NARC amesema mara tu Ruro alipoapishwa baada ya uchaguzi, Baraza la mawaziri la Kenyatta lilikuwa tayari limevunjwa na azimio lolote lililopitishwa na mawaziri hao haliwezi kuwa msimamo wa serikali.
Amesema, hatua hiyo inasalia kuwa isiyo ya kawaida kwani hakukuwa na baraza la mawaziri halali wakati uamuzi huo, huku akihoji sababu za kuagiza mahindi kutoka nje wakati ambapo wakulima wa ndani wanavuna na kwamba hatua hiyo ya haraka inaweza kuwa kashfa nyingine ya kusubiri akitolea mfano tukio la Muungano Mkuu wakati Rais akiwa Waziri wa Kilimo.
Aidha Karua amefafanua kuwa, “Mahindi, chanzo cha mlo wa kila siku kwa Wakenya walio wengi, mara nyingi huagizwa kutoka nje kwa gharama ya mkulima wa ndani na katika serikali kuu ya muungano kama waziri wa kilimo, William Ruto aliwahi kuhusishwa na Kashfa ya mahindi.
Uamuzi wa kuidhinisha matumizi ya vyakula vya GMO, ulifanywa na Baraza la Mawaziri Oktoba 3, 2022, wakati Rais Ruto alipoongoza mkutano uliowaleta pamoja wajumbe wa Baraza la Mawaziri la Uhuru katika Ikulu na sasa Kenya inapanga kuagiza magunia milioni 10 ya mahindi ya GMO katika juhudi za kulinda mapato ya wakulima ambayo yataweka msingi wa mikutano zaidi ya mfumuko wa bei.
KKA ya kuidhinisha bidhaa za GMO na uagizaji wa mahindi nchini imezua mjadala mkali nchini na wabunge zaidi wameendelea kupinga hatua hiyo wakisema haileti maana na badala yake mahindi yaagizwe nchi za Afrika hara zilizo jirani za Uganda Rwanda au Tanzania.