Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake nchini (TWFA), Amina Karuma anatarajiwa kuhudhuria kuhudhuria kongamano la viongozi wa soka la wanawake duniania litakalofanyika Zurich nchini Uswisi Septemba 28 – 02 Oktoba, 2015.

Kongamano hilo linashirkisha viongozi 35 wanawake wa mpira wa miguu kutoka semehu mbalimbali duniani ikiwa ni muendelezo wa kongamano liliofanyika mwezi Machi mwaka huu Vancouver Canada wakati wa fainali za kombe la Dunia la Wanawake.

Programu hiyo ya viongozi wa wanawake ni sehemu ya mikakati ya FIFA ya kuongeza idadi ya viongozi wengi wa soka wanawake duniani katika utawala wa mpira wa miguu wa wanawake.

 

Twiga Stars Kujipima Kwa Malawi
Joto La Mpambano Wa Simba Na Yanga