Maafisa wa Polisi wapatao 1,000 wamesimamishwa kazi na wengine kuwekewa masharti katika majukumu yao, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kulisafisha Jeshi la Polisi la mji mkuu wa London, linalokabiliwa na kashfa.
Kikosi hicho, ambacho ni kikubwa nchini humo kimekabiliwa na mlolongo wa kashfa ambazo zimedhoofisha imani ya raia kwa Polisi wa Uingereza.