Mahakama ya kesi za ufisadi nchini Uganda, imeagiza kuendelea kuzuiliwa kwa Waziri wa Serikali, Mary Gorette Kitutu na kaka yake, wanaokabiliwa na tuhuma za kutumia vibaya mali ya umma, na kuisababishia hasara Serikali.

Waziri huyo na Kaka yake, walifikishwa Mahakamani wakituhumiwa kuiba mabati yaliyokuwa yatumike kuzisaidia familia masikini katika eneo la Karamoja na wote walishtakiwa kwa makosa mawili ya kuisababishia hasara serikali na kupanga njama za udanganyifu.

Mary Gorette Kitutu akifikishwa mahakamani jijini Kampala, Picha ya The Herrald.

Kufuatia agizo hilo, Mary kaka yake wamerudishwa rumande hadi April 12, 2023 kesi hiyo itakapotajwa tena ili kusikiliza kesi hiyo inayowahusisha maofisa wengine wajuu Serikalini, na kuzua mjadala mkubwa nchini humo.

Wengi wa Wananchi na vyombo mbalimbali vya Hbari nchini Uganda, kupitia vyanzo mbalimbali wameikashifu Serikali kufumbia macho vitendo vya rushwa na kushindwa kumudu mambo ya msingi hasa kupanda kwa gharama za maisha.

Mchakato Manchester United wafufuka upya
Kocha Geita Gold akataa uteja kwa Young Africans