Imelezwa kuwa Tanzania imefikia hali ya kupungua kwa kasi ya magonjwa ya mlipuko hususani kipindupindu hapa nchini ndani ya miaka 5.

Hayo yameelezwa na BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC ambapo limesema kuwa kupungua huko kumetokana  kumetokana na usimamiaji mzuri wa sheria na kanuni za mazingira.

 Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa NEMC, Dk. Samuel Gwamaka, amesema kuwa utoaji wa elimu hasa katika kipindi cha awamu ya tano ni moja ya sababu pia amewapongeza  Watanzania kwa  kuweka mazingira safi na salama bila ya shuruti .

 â€œNEMC katika kipindi cha miaka mitano tumetoa elimu kupitia vyombo vya habari na kuandaa mikutano mbalimbali ya wadau wa mazingira na wananchi kwa ujumla wake. Tumepata mafanikio makubwa kwani takwimu zinaonesha magonjwa ya milipuko kama kipindupindu kasi ya kuenea kwake imepungua sana, sikumbuki kama tumekumbana na kipundupindu miaka mitano iliyopita,’’ alisema.

Dk. Gwamaka aliongeza kwamba chanzo kikubwa cha magonjwa ya milipuko nchini ni utiririshaji wa maji taka katika maeneo ya makazi ya watu pamoja na maji ya kemikali zenye sumu kutoka viwandani ambayo huelekezwa katika mito na makazi ya watu.

 â€œMafanikio yaliyopatikana yametokana na ushirikiano tuliopata kutoka Serikali Kuu mpaka Tamisemi, TMDA, Taasisi zote za elimu, Shirika la Viwango (TBS) pamoja na wananchi kwa ujumla. Tutaendelea kusimamia kanuni na sheria za mazingira ili ziwaletee tija Watanzania,’’ alisema.

Alisema kutokana na mwitiko chanya wa wananchi, NEMC imeunda kikosi kazi cha dharura ambacho kinafanya kazi kwa saa 24 ambapo kazi yake ni kuhakikisha changamoto za kimazingira zinashughulikiwa kwa wakati.

Gwajima, Pengo, Makonda Uso kwa Uso
Amuua mwanae akitaka kujua jinsia