Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amemuapisha Balozi Batilda Salha Burian kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora pamoja na Zuwena Omari Jiri kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga.

Uapisho huo umefanyika leo Juni 21, 2021 Ikulu Jijini Dodoma ambapo uapisho huo umehudhuriwa na Waziri Mkuu Kassim Mjaliwa, Waziri wa TAMISEMI.

Waziri Ummy Mwalimu amesema mmoja ya kazi aliyonayo Mkuu wa Mkoa mpya wa Tabora ni kuhakikisha halmashauri zinafanya vizuri kwani changamoto iliyopo katika mkoa huo ni ukusanyaji wa mapato katika halmshauri.

Balozi Batilda Salha Burian ameapishwa kuwa Mkuu wa mkoa wa Tabora leo ikulku Dodoma, akichukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa mkoa huo Ally Hapi ambaye alihamishiwa mkoa wa Mara.

LHRC waingilia kati swala la mtoto aliyeungua moto
Ukarabati viwanja fursa kwa vijana