Mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi amesema kuwa vyama vya upinzani vimekosa hoja yenye mashiko ambayo inaweza kuleta ushawishi kwa jamii.
Ameyasema hayo hii leo Jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa vyama vya upinzani vimepoteza muelekeo kutokana na vyama hivyo kuwa mali ya watu badala ya kuwa taasisi imara kwa maslahi ya wananchi.
Amesema kuwa kabla ya kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) alikuwa Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha) na kutokana na ubabaishaji aliouona akiwa Chadema ulimfanya aondoke.
Aidha, amesema kuwa wanasiasa wengi ambao wanaondoka upinzani na kujiunga CCM inatokana na utendaji wa Rais Dkt. Magufuli katika kuwatumikia Watanzania na wala si kosa kuunga mkono jitihada zinafanywa na Serikali ya Awamu ya Tano.
“Kuunga mkono juhudi za Rais si kosa ,ndio maana binafsi nimeamua kuwa mzalendo kwa kuamua kuwa mkweli pale ambapo Serikali inafanya vema lazima niwe mkweli kwa kusifu na kupongeza bila woga.Hivyo sitaogopa kuunga mkono juhudi hizo.
Hata hivyo, ameongeza kuwa changamoto kubwa iliyopo kwa vyama vya upinzani ni kwamba vingi vimekuwa kama kampuni za watu kwa ajili ya kufanikisha maslahi yao.
-
Wasira amtaja mchawi wa CCM
-
Mbowe: CCM bila Polisi ni wepesi
-
Video: CUF, Chadema watunishiana misuli Kinondoni