Mkazi wa kijiji cha Kamalampaka mkoani Katavi, John Kipindapinda ameuawa kwa kupigwa fimbo kichwani na wanawake wawili waliodai alitaka kuwabaka.

Tukio hilo limebainishwa na mkuu wa wilaya ya Mlele, Rachel Kasanda, jana alipokuwa akitoa taarifa ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo mbele ya mkuu wa mkoa wa Katavi Juma Homera wakati wa ziara yake.

Kasanda wamesema mtuhumiwa huyo aliuwa wiki iliyopita nyumbani kwa Christina Said wa kijiji cha Kamalampaka majira ya usiku.

Amesema siku ya tukio, Christina alikuwa amelala chumbani kwake akiwa na mwanamke mwenzake aliyetajwa kwa jina moja la Saida, ghafla aliingia mtuhumiwa huyo katika chumba chao huku akijifanya amelewa.

Wakati mtuhumiwa huyo ambaye ni marehemu kwa sasa, akianza kuwavamia, wanawake hao walimuwahi na kuanza kumshambulia kwa fimbo kichwani huku wakipiga kelele kuomba msaada kutoka kwa majirani.

Majirani walipofika walikuta mtuhumiwa amejeruhiwa kichwani, walimchukua na kumpeleka kituo cha polisi cha wilaya ya Mlele kisha kumpeleka kituo cha afya Inyonga ambako alifariki.

Mkuu wa mkoa huo ametoa wito kwa wakazi kuacha tabia ya kuuana hasa katika kipindi hiki cha mavuno kwani takwimu zinaonesha kuwa wakti huu ndipo matukio mengi ya mauaji hutokea.

Waziri Mkuu ataja idadi mpya ya wagonjwa wa corona
Wizara yaagiza samaki kuwekewa alama kabla ya kuuzwa nje ya nchi