Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, (CCM) Dkt. Bashiru Ally Katika mwendelezo wa mahojiano aliyoyafanya na Raia Mwema, amemnyooshea kidole, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa namna anavyotekeleza majukumu yake ya ukuu wa Mkoa na kudai kuwa kulikuwepo udhaifu katika kushughulikia makontena kutokana na kufanya kazi bila kushirikishana.

Amesema kuwa, Mkuu wa Mkoa alipaswa kuwashirikisha wenzake tangu hatua za awali, kwa kuwa Serikali ni moja, hakuna cha Waziri wala Mkuu wa Mkoa kwakuwa wote ni Wateule wa Rais.

Aidha, Dkt. Bashiru amemnyooshea kidole Makonda kwa ubinafsi na kukumbushia jinsi ambavyo mkoa wa Dar es Salaam ni mojawapo ya Mikoa aliyoitaja hivi karibuni kwa kutotekeleza vyema Ilani ya CCM kutokana kufanya kazi bila ushirikiano.

“Hapa sina maana kwamba ni Mkuu wa Mkoa tu hapana, ni uongozi mzima chini ya Mkuu wa Mkoa na uongozi mzima chini ya Mwenyekiti wa Chama.”amesema Dkt. Bashiru

Sauti ya Hamisa yaibua makubwa ya Wema, Mange avujisha siri nzito
Akutwa na Vijiko, Viberiti, Mswaki, tumboni