Katibu mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mary Makondo amewataka wanavyuo kuvaa mavazi yenye staha na yanayozingatia maadili ili kuwa kioo chema kwa jamii inayowazunguka.

Ameyasema hayo katika mahafali ya 38 ya Chuo cha Ardhi Tabora, baada ya kuwaona baadhi ya wahitimu wa kike wakiwa wamevaa nguo zisizo na staha.

”Mimi kama mzazi niseme tuu tuangalie tulivyo walimu wametufundisha tumepata elimu muda tuliokaa tubadilike, namna mlivyovaa inakuonyesha ulivyo,” amesema Katibu mkuu Makondo.

”Hata tukisema mtoa majoho sasa hivi ni aibu tupu, wengi mtaaibika lazima mbadilike mvae vizuri’,’ ameongeza.

Aidha, Katibu Mkuu amesema kuwa baadhi ya wahitimu nguo walizovaa zinaweza zikawakosesha ajira kwa kuwa ni kielelzo cha jinsi walivyo na hata wakipewa kazi ndivyo watakavyokuwa.

Katibu mkuu Makondo amewataka wanafunzi wataopata fursa ya ajira kuwa waadilifu na wazalendo na kuepuka tamaa ya kupata utajiri wa haraka ambao utawasababishia kuishia kifungoni.

Kocha Sven aeleza Simba SC 'itakavyoipiga' FC Platinum
Chanzo kifo cha Askofu Banzi

Comments

comments