Katibu Mkuu wa Halmashauri ya Shirika la Ukombozi wa Palestina (PLO), Dkt. Saeb Erekat aliyefariki Novemba 10, baada ya kukutwa na virusi vya corona (Covid-19), amefanyiwa mazishi ya safari yake ya mwisho katika Ukingo wa Magharibi.

Mwili wa Erekat uliokuwa ukihifadhiwa katika hospitali ya Hadassah iliyoko Jerusalem ya Magharibi ya Israel, ulisafirishwa leo hii hadi Ukingo wa Magharibi kwa ajili ya shughuli ya mazishi iliyoandaliwa mjini Ramallah na mamlaka ya rais wa Palestina.

Shughuli hiyo ya mazishi ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa ngazi za juu za serikali ya Palestina akiwemo Rais Mahmud Abbas na Waziri Mkuu Muhammed Ishtiyya.

Baada ya shughuli ya mazishi, jeneza la Erekat lilisafirishwa hadi mji wa Eriha kutoka Ramallah na mwili wake mwili wake kuswaliwa katika msikiti wa Tarihi Eriha ambapo maelfu wa wananchi wa Palestina walijumuika.

Baadaye mwili wa Erekat ukasafirishwa kutoka msikitini na kuzikwa katika eneo la makaburi ya Al-Babayi mjini Eriha.

Erekat aliwahi kufanyiwa upandikizaji wa mapafu mwaka 2017 nchini Marekani.

Oktoba 8 alilazwa hospitali baada ya kukutwa na ugonjwa wa Covid 19 ambapo baada ya hali yake afya kuwa mbaya, alisafirishwa tarehe 23 Oktoba kutoka kwenye nyumba yake mjini Eriha, Ukingo wa Magharibi na kulazwa katika hospitali ya Hadassah iliyoko Jerusalem Magharibi ya Israel mpaka alipokutwa na umauti.

Mwanasiasa huyo mkongwe wa Palestina aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 65, alikuwa mstari wa mbele katika kusimamia mazungumzo ya kutafuta suluhuhiso katika mzozo kati ya Palestina na Israel.

Bunge lawakubali Majaliwa, Tulia
Rais Magufuli amteua Majaliwa kuwa Waziri Mkuu