Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni, Profesa Elisante Ole Gabriel amewasili leo visiwani Zanzibar kuhudhuria kilele cha Tamasha la Kimataifa la Filamu (ZIFF).
Profesa Elisante ambaye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha tamasha hilo la kimataifa, amewasili katika viunga vya Ngome Kongwe visiwani humo akiongozana na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fisoo na kufanya mkutano na waandishi wa habari.
Tamasha la ZIFF ambalo mwaka huu lilifunguliwa rasmi Julai 8, linasherehekea miaka 20 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1998.
Tamasha la ZIFF husaidia kutangaza filamu hususan za Afrika katika soko la nyumbani na soko la kimataifa na huwakutanisha wasanii na wadau wa sanaa kwa ujumla kutoka nchi mbalimbali.
- Tazama hapa matokeo kidato cha sita (ACSEE), ualimu (DSEE) na GATCE 2017
- Rais wa Brazil kikaangoni, Bunge lamkingia kifua
Mwaka huu, pamoja na mambo mengine, tamasha hilo limeongeza kipengele cha tuzo ya video bora ya muziki kutoka Afrika Mashariki yenye lengo la kuutangaza muziki wa kizazi kipya uliofanyika ndani ya Jumuiya ya Affrika Mashariki na kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania.