Kasi ya Rais John Magufuli imewashinda baadhi ya watendaji akiwemo Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Mhandisi Madeni Juma Kipande ambao wamewekwa kando.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amesema kuwa Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mhadisi Kipande ambaye alikuwa akisubiri muda wa kuthibitishwa, baada ya kutoridhishwa na utendaji wake.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemrejesha nyumbani Balozi wa Tanzania aliyeko London, Balozi Peter Allan Kallaghe. Amemtaka arudi katika wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambapo atapangiwa kazi nyingine.

Wakati Balozi huyo akiondolowa, Rais amemtuuwa Mahadhi Juma aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa serikali ya awamu yanne, kuwa Balozi wa kwanza wa Tanzania nchini Kuwait.

Pia, Rais ameamuru kuwa mabalozi wawili waliomaliza mikataba yao kurudi nyumbani. Mabalozi hao ni Batilda Salha Buriani, aliyeko Tokyo, Japan na   Dkt. James Alex Msekela, aliyeko Rome, Italia.

Diamond autaka uwaziri wa Nape
Rais Magufuli amtimua Mkurugenzi wa NIDA, Mabilioni yalitumika ndivyo sivyo