Katibu anayeshughulikia vyombo vya habari wa Ikulu ya Marekani, Sean Spice amejiuzulu nafasi hiyo leo akipinga uamuzi wa Rais Donald Trump kumteua mkurugenzi mpya wa mawasiliano.

Spicer amepinga vikali uteuzi wa Antony Scaramucci ambaye atafanya sehemu ya majukumu aliyokuwa akiyafanya, akidai kuwa ni kosa kubwa lililofanywa na rais Trump na kwamba ameichafua timu yake ya mawasiliano.

Hatua hiyo ya Spicer ni pigo kwa Ikulu ya Marekani katika wakati huu ambapo imekuwa ikiandamwa na vyombo vya habari kwa kashfa ya kujihusisha na Urusi kuingilia uchaguzi wa nchi hiyo uliomuingiza madarakani Rais Trump.

Spicer alikuwa anafahamika kwa jinsi alivyoweza kupangua hoja za wanahabari lakini alianza kupotea hadharani katika kipindi cha wiki mbili zilizopita.

Mchakato wa kumpata mkurugenzi wa habari wa ‘White House’ ulianza baada ya Mike Dubke kujiuzulu nafasi hiyo mwezi Mei mwaka huu.

Kutokana na hatua hiyo ya Dubke, Spicer alikuwa anafanya kazi kwa wakati mmoja kama katibu anayeshughulikia vyombo vya habari pamoja na mkurugenzi wa mawasiliano.

 

Video: Mwanasheria wa Tundu Lissu agonga mwamba, ashindwa kuonana na mteja wake
Majaliwa awataka NHC kujenga nyumba katika maeneo mengine ya utawala