Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi ya CCM, Abdallah Bulembo amesema chama chake hakitawaruhusu wapinzani kuingia Ikulu.

Akiongea katika mkutano wa kampeni wa chama hicho jana, Bulembo alieleza kuwa chama chake kiko tayari kufanya kila kitu lakini sio suala la kuwaruhusu wapinzani kuingia Ikulu.

“Hatuwezi kuwaruhusu kwenda ikulu.. hilo hatufanyi, mengine yote tutafanya , lakini kuwaruhusu waende ikulu hilo hatufanyi,” alisisitiza Bulembo.
 

Kauli hiyo imepokelewa kwa hisia tofauti na wafuatiliaji wa mambo ya kisiasa ambapo baadhi wameeleza kuwa kauli hiyo haikuwa sahihi katika nchi ya kidemokrasia.

Jerome Valcke Asimamishwa Kazi FIFA
Girlfriend Wa Mtoto Wa Will Smith Sio ‘Msafi’ Kama Anavyoonekana