Walimu Wakuu wa Shule za Msingi Mlimani na Tunduma TC ambao awali walivuliwa vyeo na kusimamishwa kazi kufuatia kipande cha Video iliyosambaa mitandaoni ikionesha Wanafunzi wakicheza wimbo wa Bongo Fleva, wamerejeshwa kazini.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri Mji wa Tunduma, Seleman Kateti amesema hatua hiyo inatokana na kauli ya Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson aliyoitoa bungeni hapo jana Novemba 6, 2023 kwamba Walimu hao wapewa nafasi ya kusikilizwa.

Amesema, Dkt. Tulia alitoa wito huo wakati akitaka ufafanuzi kwa Waziri wa Elimu, Prof. Adolf Mkenda akisema kama Walimu hao hawakuwepo Shuleni na Mamlaka ya Nidhamu imechukua hatua kabla ya kufanya uchunguzi, basi Walimu hao warejeshwe kwenye nafasi zao.

Awali, Prof. Mkenda alisema endapo adhabu hiyo haikuwatendea haki Walimu hao wanaodaiwa kutokuwepo Shuleni siku ya tukio, wanatakiwa kukata rufaa jambo ambalo lilipingwa na Spika Tulia akidai haiwezekani mtu kukata rufaa wakati alihukumiwa bila kusikilizwa.

Msifanye shughuli za kibinadamu kwenye kingo za Mito - Serikali
Ben White kulipwa mara mbili Arsenal