Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Charles Kichere amefunguka na kusema wamepanga kumchunguza kiongozi wa dini Askofu Zakary Kakobe kufuatia kauli yake aliyotoa katika mahubiri aliyofanya siku ya krismasi na kudai kuwa ana pesa nyingi kuliko serikali.

“Kama mtu ana hela kuliko serikali, kama ambavyo tunajua serikali yetu inatoa huduma inanunua ndege, imejenga standard gauge, inajenga barabara, inatoa elimu bure, inalipa mishahara kwa watumishi wa umma, inalipia madawa hospitalini, inalipa na kutoa huduma za ulinzi na usalama kwa wananchi’’ Amesema Kichere.

Hata hivyo TRA imesema hakuna kumbukumbu za ulipaji kodi wa Askofu Kakobe baada ya kupitia  kumbukumbu zao juu ya ulipaji kodi wake.

“Kuna Matajiri tunawafahamu lakini hawaizidi serikali kwa pesa, tumeona wamekuwa wakilipa kodi na kuonekana kwenye kumbukumbu zetu lakini huyu tajiri Askofu Kakobe si miongoni mwao’’.

Aidha TRA wamemtaka Askofu Kakobe kutoa ushirikiano ili wajiridhishe juu ya utajiri wake na ulipaji kodi wake.

 

Nchemba atoa agizo zito, umiliki wa kitambulisho cha Taifa
TCRA yashusha gharama za kupiga simu