Mbunge wa Viti maalumu Chadema, Devotha Minja leo katika mkutano wa 15 kikao cha 6 ameuliza swali la nyongeza na kuhoji juu ya makamanda wa polisi wanaotumia lugha za vitisho kwa wananchi.

Minja amehoji kazi ya msingi ya jeshi la polisi kwa wananchi wanaolipa kodi ni kuchakazwa.

Hayo yamejiri kufuatia kauli iliyotolewa jana na kamanda wa polisi Dodoma, Giles Muroto ambaye alitoa tahadhari kwa wananchi ambao leo April 9, 2019 walipanga kufanya maandamano ya amani kupinga azimio la bunge kuhusu kufanya kazi na CAG.

”Si wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya tu ambao hawafanyi vizuri wapo pia ma RPC ambao hawafanyi vizuri, mwenyekiti RPC anapotangaza kwamba wananchi wakiandamana atawapiga hadi wachakazwe, hivi kazi ya msingi ya jeshi la polisi kwa wananchi wanaolipa kodi ili walipwe mishahara kazi ya msingi ni kuchakaza wananachi”.Amehoji Devotha Minja

Akijibu swali hilo Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo amesema kuwa kila nchi inaendeshwa kwa kanuni na sheria ambazo ni lazima zifuatwe na watu wote bila shuruti, hivyo amewaomba wananchi kufuata sheria hizo ili kujikinga kuingia mikononi mwa polisi au kulazimisha polisi kutumia nguvu.

”Nadhani kitu kikubwa kama taifa ni kuweka ushirikiano katika kila eneno nadhani vyombo vingine vinaongozwa kwa mujibu wa sharia kanuni na taratibu hasa kjatika suala zima la mambo ya ndani. Wananchi wote tutafuata utaratibu wa utii wa sharia na taratibu bila shuruti” amejibu Jafo.

 

 

Drake, Wizkid ndani ya jukwaa moja
LIVE: Rais Magufuli akihutubia wananchi wa Madaba - Ruvuma

Comments

comments