Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amewataka watanzania kutoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama punde tu wanapoona viashiria vya ujambazi ili viweze kufanya kazi iliyokusudiwa na kutokomeza vitendo hivyo.

Aidha amesema kuwa Serikali inahakikisha usalama wa raia na mali zao unaendelea kuwepo.

Kauli hiyo ameitoa leo Mei 27, 2021, Bungeni Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa Makete Festo Sanga, lililohoji ni nini kauli ya serikali kufuatia vitendo vya ujambazi vilivyochipukia siku za hivi karibuni katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya na Dodoma.

“Jeshi la Polisi linafanya kazi nzuri sana siku mbili tatu nimesikia kazi nzuri waliyoifanya Dar es Salaam kudhibiti majambazi nataka niwahakikishie serikali inaendelea na kazi hiyo kuhakikisha ulinzi unaendelea” amesema Waziri Mkuu

Biden ataka chanzo cha corona kuchunguzwa upya
Wachezaji Young Africans wapumzishwa