Inaelezwa kuwa aliyekua Kocha Mkuu wa Young Africans Cedrick Kaze huenda akarejea klabuni hapo kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye benchi la ufundi.
Kaze alikuwa ndani ya Young Africans msimu uliopita (2020/21) ambapo hakuweza kukamilisha mzunguko wa pili baada ya mabosi wa timu hiyo kuamua kumfungashia virago.
Kwa mujibu wa Young Africans walieleza kuwa Kaze alishindwa kuwapa kile ambacho walikuwa wanafikiria jambo ambalo liliwafanya waweze kufikia makubaliano ya kuachana naye.
Mechi yake ya mwisho alishuhudia vijana wake wakigawana alama dhidi ya Polisi Tanzania na bao la Young Africans lilifungwa na mchezaji Fiston Abdulazak ambaye kwa sasa hayupo ndani ya kikosi hicho.
Taarifa zimeeleza kuwa Kaze anarejea klabuni hapo akiwa ni kocha msaidizi huku Kocha Mkuu akibaki kuwa Nasreddine Nabi.