Kocha Mkuu wa Namungo FC, Cedric Kaze amesema kuwa watazidi kuwa imara taratibu kutokana na maandalizi ambayo wanayafanya kwenye mechi zao zote za ligi.

Timu hiyo ilianza kwa kupoteza mchezo wa kwanza wa ligi dhidi ya JKT Tanzania kwa kufungwa bao 1-0 na mchezo wa pili ilipata sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya KMC.

Kaze amebainisha kuwa kuna ushindani mkubwa ndani ya ligi jambo linalowafanya wazidi kujiimaraisha kila wakati.

Kocha huyo kutoka nchini Burundi amesema: “Kuwa bora ni mchakato ambao unafanyika na unahitaji muda hilo ni jambo ambalo tunalihitaji kwa namna hali ilivyo kila siku kunakuwa na mabadiliko kwa kuwa makosa tunayafanyia kazi.

“Mchezo wa kwanza kuna mazuri tulifanya na mabaya tuliyokosea hayo yote ni muhimu kwetu kuyachukua na kufanyia kazi kuwa imara kwenye mechi zinazofuata ligi inaanza nasi tunazidi kupambana kuwa imara.”

Ahmed Ally: Tuna imani na Robertinho
Watoto 500 wafariki kwa njaa Sudan mapigano yakiendelea