Serikali Nchini, imeitaka Menejimenti ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini – KCMC, kuimarisha ushirikiano, ili kuboresha Huduma za afya wanazozitoa kwa wananchi

Wito huo, umetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel wakati alipokutana na Menejimenti ya Hospitali hiyo na kuwa pongeza kwa kazi nzuri wanayofanya ya kuhudumia wananchi.

Amesema, “kufikia ubora wa Huduma katika Hospitali hii lazima muwe na ushirikiano wa katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuleta matokeo chanya kwa wananchi wanao fata Huduma hapa.”

Naye Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini KCMC, Prof. Gileard Masenga amemshukuru Dkt. Mollel kwa ujio wake na kuwatia nguvu katika kuendelea kutoa Huduma katika hospitali hiyo.

Umeme si anasa ni hitaji la lazima - Dkt. Biteko
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Septemba 29, 2023