Katibu wa Baraza la Usalama la Ukraine Alexey Danilov amesema Jumanne kuwa Kiev inakusudia kurusha makombora yake katika nchi jirani ya Belarus kwa madai kuwa wanajeshi wa nchi hiyo wanashiriki operesheni ya kijeshi iliyoanzishwa na Urusi.

“Ikiwa ni lazima, ikiwa Amiri Jeshi Mkuu atafanya uamuzi kama huo, tutafanya,” Danilov aliambia shirika la utangazaji la Ukraine 24.

Tishio hilo linakuja huku kukiwa na madai ya mara kwa mara ya wanajeshi wa Belarus kushiriki katika operesheni ya kijeshi inayoendelea dhidi ya Ukraine iliyoanzishwa na Urusi wiki iliyopita.

Hakuna ushahidi thabiti wa kuhusika kwa Belarusi, hata hivyo, tuhuma zimeibuka na Minsk ikisisitiza kuwa haijahusika katika operesheni hiyo.

Msimamo huo ulisisitizwa na Rais wa Belarus Alexander Lukashenko mapema Jumanne, ambaye alisema kuwa wanajeshi wote wa nchi hiyo wanasalia katika vituo vyao vya kudumu.

Wakati huo huo, Lukashenko alionya dhidi ya vitisho kwa nchi yake, akionya kwamba Belarus iko tayari kujilinda ikiwa ni lazima.

Tangazo la BurjKhalifa halijalipiwa
Geita waidai TAMISEMI V8 yao ya Mil. 400