Rapa Kendrick Lamar amedhihirisha kuwa huenda akawa ndiye mfalme wa tuzo za Grammy za mwaka 2016 baada ya kuongoza kwa kutajwa kwenye vipengele 11.

Kendrick amefunika kwenye orodha ya wanaowania tuzo hizo huku akigusa pia kwenye tuzo kubwa zaidi. Albam yake ya ‘To Pimp a Butterfly’ imetajwa kuwania tuzo ya albam bora ya mwaka huku wimbo wake ‘Alright’ ukitajwa kati ya nyimbo bora za mwaka.

Lamar amevunja rekodi za tuzo hizo japo hajaifikia rekodi ya Mfalme wa Pop, Michael Jackson ambaye aliwahi kutajwa katika vipengele 12 na kuondoka na tuzo nane kwa usiku mmoja wa tuzo.

Q – Chillah Adai Kifo Chake Kitaongeza Thamani Ya Muziki Wake
Ronda Rousey aelezea maumivu ya Kipigo cha Holm, ‘Siwezi Kutafuna tunda’