Mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Uvinalies Nyabuto, amekamatwa na kutiwa mbaroni kwa kosa la kusimamisha msafara wa magari wa Rais Uhuru Kenyatta katika barabara ya kuelekea ikulu jana.
Imeelezwa kuwa Nyabuto alisimamisha msafara akiwa ameshika bango lililoandikwa “Mheshimiwa tafadhali naomba nafasi ya kujiunga na majeshi ya ulinzi. Nisamehe kwa kutoheshimu ulinzi wako. samahani Rais. Nyabuto”
Kwa mijibu wa Polisi, msafara huo ulikuwa unaelekea Ikulu ukitokea ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Kenyatta (KICC) ambapo Rais Kenyatta alitoka kwenye mkutano wa 9 wa wakuu wa nchi za Caribbean na Pacific.
Sudan kuwalipa waathiriwa wa mabomu ya Osama, Kenya na Tanzania ya mwaka 1998
Hata hivyo jitihada zake za kukutana na Rais ziligonga mwamba, alikamatwa na walinzi walio kwenye msafara wa Rais na baadaye alipelekwa katika kituo cha polisi kilimani ambapo aliendelea kushikiliwa.