Nchini Kenya Inspekta Jenerali wa Polisi, Hilary Mutyambai amewaagiza Polisi kumkamata mtu yeyote atakayeonekana mitaani bila kuwa na Barakoa.
Amesema kuvaa Barakoa ni lazima ili kuzuia maambukizi ya Covid 19 na kutovaa ni kosa linaloweza kupelekea kutozwa faini Laki 4 au ya kifungo cha miezi 6, au vyote kwa pamoja.
Aidha amewataka wafanyabiashara kuweka sabuni na maji kwa ajili ya wateja au vitakasa mikono vilivyothibitishwa na shirika la viwango la Kenya.
Dar: Serikali yataja hospitali 25 zilizotengwa kwa COVID 19
Pia, wametakiwa kuhakikisha wateja wanaachiana nafasi isiyopungua mita 1 na watakaokiuka tangazo hilo watalipa faini ya takriban Tsh laki 4 au kifungo cha miezi 6 au vyote.
Pamoja na hayo, Wizara ya Afya imewataka waendesha bodaboda kubeba abiria mmoja tu kwa safari.