Mahakama jijini Nairobi imemuachia kwa dhamana Gavana wa Nairobi, Mike Sonko aliyetiwa mbaroni siku 5 zilizopita huku akipewa masharti ya kutokwenda ofisini.

Dhamana yake ametakiwa kulipa Ksh. Milioni 15 pesa tasilimu au kuweka bondi vitu vyake vyenye thamani ya Ksh. Milioni 30.

Hapo awali gavana huyo anayeshtakiwa kwa makosa zaidi ya 30 yakiwemo ya utakatishaji fedha na rushwa, aliomba kuachiwa akieleza nafasi yake kwenye jamii na kueleza kuwa anahitaji matibabu.

Aidha Mahakama imemtaka Sonko kutotumia ofisi yake na endapo atahitaji vitu vyake ofisini atasindikizwa na maafisa upelelezi lakini pia hatakiwi kusema lolote kuhusu kesi hiyo kwenye mitandao ya kijamii.

Halikadharika Mahakama imemtaka kukusanya nyaraka zake za kusafiria na kumtaka kuzuia mashabiki wake kutozua vurugu wakati kesi yake inaposikilizwa.

Kocha Stars afungiwa CECAFA
Nyumba za kulala wageni 'guest house' zachangia mfumuko wa bei

Comments

comments