Ripoti ya Bureau of International Narcotics and Law Enforcement Affairs imeitaja Kenya kuwa Kitovu cha Utakatishaji Fedha ambao hufanyika kwa Taasisi rasmi na zisizo rasmi katika eneo la Afrika Mashariki.

Aidha, Kenya imetajwa kuwa na wafadhili wa ugaidi, vikundi vya uhalifu wa kimataifa, uhalifu wa mtandaoni, uharamia na biashara haramu ya mali pori.

Ripoti hiyo imetaja kuwa ukaribu wa Kenya na Somalia kijiografia kunaifanya nchi hiyo itumike zaidi kwa Biashara haramu na kuwa njia kuu ya Dawa, kuuza watu na wanyama pori.

Aidha, ripoti hiyo imeisifia Tanzania kwa kuwa na Sheria ya kudhibiti Utakatishaji Fedha huku ikitajwa kuwa na changamoto ya kitaasisi kudhibiti Ukwepaji Kodi na Rushwa.

Luis Miquissone: Simba SC imebadilisha maisha yangu
Wananchi wazuiwa kuchukua mchanga wa kaburi la Maalim Seif