Padri wa kanisa katoliki nchini Kenya aliyekuwa ametoweka kwa siku saba baada ya kutekwa, mwili wake umepatikana ukiwa umefukiwa kwenye kingo za mto.

Kwamujibu wa taarifa zilizotolewa na jeshi la polisi, imeelezwa kuwa mwili wa Padri Michael Maingi Kyengo (43), ulipatikana baada ya moja ya watuhumiwa kuwaelekeza polisi siku ya jumanne, aneo walilo fukia mwili huo.

Lissu apigilia msumari kugombea urais 2020

Imeelezwa kuwa Padri huyo alitoweka kutoka kanisa la Thatha lililopo Machakos Oktoba 8 mwaka huu, na imeelezwa kuwa kwa mara ya mwisho aliondoka hapo na gari lake lakini hakurejea tena.

Video: Nape achomoza kivingine, Lissu asisitiza kugombea Urais

Mwili wake umechukuliwa na jeshi la Polisi na kupelekwa hospitali kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi zaidi.

Kamanda wa polisi, Daniel Rukanga, amesema ” Tunataka kufanya uchunguzi kwenye mwili wake ili ukweli ubainike, na tutatafuta chanzo cha mauaji haya kwa kuendelea na uchunguzi kwa watuhumiwa wote walio husishwa na mauaji ya kiongozi huyu”

 

LIVE: Yanayojiri katika ziara ya Rais Magufuli Lindi
Lissu apigilia msumari kugombea urais 2020