Watu 60 wamejeruhiwa baada ya kukanyagana wakati wakilazimisha kuingia katika uwanja wa Kasarani kushuhudia uapisho wa Rais, William Ruto huku wakilishutumu Jeshi la Polisi kwa kuwashambulia wakidai hakukuwa na ulazima wa kufanya hivyo.
Mganga wa Hospitali ya jiji la Nairobi, Peter Muiruri amethibitisha kupokea majeruhi hao na kusema wengi wa majeruhi hao walikuwa na majeraha madogo na walipatiwa matibabu na kuruhusiwa huku akidai kuwa hakuna ripoti ya kifo.
Amesema, “Idadi ni kubwa ya watu waliojeruhiwa na ilitubidi kuwatibu wengine waliokuwa na majeraha madogo ila wengi wao walikimbizwa katika hospitali kuu ya jiji Nairobi na ja,bp la kushukuru ni hakukuwa ripoti za vifo.
Watu hao, wanadaiwa kujaribu kukwepa vikosi vya usalama vilivyokuwa na virungu, huku baadhi yao wakishindwa na kudai walipigwa na polisi baada ya kujaribu kuingia ndani ambapo mtu mmoja Benson Kimutai akisema Polisi walitumia nguvu.
Uapisho wa Ruto, umefanyika baada ya kushinda uchaguzi wa Agosti 9 dhidi ya mshindani wake kiongozi wa muda mrefu wa upinzani, Raila Odinga, uchaguzi uliofanyika kwa demokrasia thabiti kuwahi kutokea Afrika Mashariki, na Mahakama ya Juu kukataa changamoto za matokeo.
Rais William Ruto, anachukua mamlaka katika nchi hiyo iliyolemewa na madeni ambayo yatapinga juhudi zake za kutimiza ahadi kuu za kampeni alizotoa kwa Wakenya na uapisho wake umefanyika rasmi Agosti 13, 2022 na kushuhudiwa na Viongozi mbalimbali Barani Afrika.