Mawaziri wa Mambo ya Nje Nchi za Kenya na Somalia zimekubaliana kushirikiana kuboresha diplomasia, biashara, elimu, kilimo, ulinzi usalama, utalii na uhusiano mwingine kati yao kufuatia miaka kadhaa ya mvutano.
Aidha taarifa ya pamoja iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Somalia imesema kuwa walikubaliana kufanya mkutano kujadili masuala yenye maslahi kwa pande zote mbili.
Hata hivyo Mawaziri wa Nchi hizo pia wamekaribisha katika hatua ya kurejea kwa mabalozi mjini Mogadishu na Nairobi.
Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi “Farmajo” Mohamed alikutana na waziri wa mambo ya nje wa Kenya na kukaribisha matokeo ya mazungumzo na kuelezea kujitolea kwake kutekeleza suala la amani na “ujirani mwema”.
Uhusiano wa Kenya na Somalia umekuwa dhaifu katika miaka ya hivi karibuni kutokana na madai ya Kenya kuingilia masuala ya ndani ya Mogadishu na pia juu ya mzozo wa mipaka ya baharini katika Bahari ya Hindi miongoni mwa masuala mengine.