Serikali ya Kenya imewaamuru makamishna wote wa Kaunti kuanza uchunguzi juu ya wanafunzi walioshindwa kuripoti shuleni na sababu zilizopelekea hilo, na kuchukua hatua za kuwarudisha.

Siku moja baada ya Shule kufunguliwa, Katibu Tawala wa Elimu, Zack Kinuthia amesema licha ya makamishna kuwa wenyeviti wa Kamati za Usalama za Kaunti lakini pia, wao ni kama jicho la rais hivyo wanapaswa kutekeleza jukumu hilo hata katika shule binafsi.

“Ni Sera ya Serikali kwamba ujauzito sio ugonjwa ambapo imetokea tumethubutu kusema sio kosa kuwa mjamzito, kosa ni jinsi ujauzito huo ulivyopatikana, hatutavumilia ubaguzi na unyanyapaa kwa Wasichana wetu ambao wanatarajia kuwa Mama”.

Kinuthia amesema wanafunzi wote wanaotakiwa kufanya mitihani yao ya Kitaifa watafanya hivyo bila kujali kama ni kinamama au wajawazito.

Aidha, Waziri wa Elimu Profesa George Magoha amewataka walimu katika shule za umma sambamba na zile za binafsi kutowarudisha nyumbani wanafunzi kwa sababu ya karo.

Waziri Magoha ametoa agizo hilo jana alipokuwa akizungumza katika shule ya msingi ya Olympic, mtaani Kibra Nairobi alipoongoza ufunguzi wa shule ambapo amesema masomo katika shule za msingi na sekondari ni ya bila malipo isipokuwa shule za bweni ambapo wazazi wanahitajika kulipa.

Serikali ya Kenya ilifunga shule zote Mwezi Machi mwaka huu baada ya Kenya kurekodi kisa cha kwanza cha Corona mpaka jana Oktoba 12 shulezilipofunguliwa.

TFF yashindwa kutoa uamuzi sakata la Morrison
Ukata wakwamisha kampeni za UDP