Serikali nchini Kenya, imefunga ofisi ya ubalozi wake mjini Khartoum – Sudan, huku kukiwa na ripoti kwamba makundi yenye silaha sasa yanalenga maafisa wa kidiplomasia.
Kwa mujibu wa Taarifa ya Katibu mkuu wa masuala ya kigeni, Korir SingOei imeeleza kuwa ubalozi wa Kenya ulikuwa wazi kuwezesha kuhamishwa kwa Wakenya wowote waliosalia katika nchi hiyo.
Hatua hiyo inakuja kufuatia kuzuka upywa kwa mapigano ambayo yameanza kufuatia kukosekana kwa muafaka baina ya pande mbili zinazokinzana za Jeshi la Serikali na lile la akiba la RSF.
Hata hivyo, Wawakilishi wa jenerali Abdel Fatah al Burhani na mwenzake Mohamed Hamdani Dagalo, bado wapo mji wa bandari wa Saudia, Jeddah, licha ya kuvunjika kwa makubaliano ya usitishaji mapigano ya juma lililopita.