Jeshi la Polisi katika kaunti ya Mandela, kaskazini Mashariki mwa Kenya limejipanga kwa tahadhari, baada ya kuripotiwa kuonekana kwa washukiwa 20, wa kundi la kigaidi la Al-shabab kutoka nchini Somalia katika eneo hilo.
Duru zinaeleza kuwa, magaidi hao walionekana katika maeneo ya Bale-Ilman na kutulo ijumaa iliyopita na inasadikika wamebeba vifaa mbalimbali vya milipuko.
Ni Kenya tena: Mwanariadha wa kike avunja rekodi ya dunia
Siku ya jumamosi maofisa 10 wa polisi nchini Kenya, walifariki baada ya gari lao kukanyaga bomu ambalo linasadikiwa kuwa lilitegwa na kundi la Al-shabab. maofisa hao walikuwa katika kambi ya Garissa.
Baada ya tukio hilo Gavana wa Garissa, Ali Korane alisema kuwa shambulio hilo ni kinyume na matakwa ya amani na ni hatari kwa usalama.
Japan: Waokoaji 110,000 watafuta waliokumbwa na kimbunga Hagibis
Kenya imeendelea kuwa kwenye vita na kundi la Al-shababu tangu mwka 2011 ilipotuma majeshi yake nchini Somalia.