Ijimaa Mei 11, 2018 wanasayansi wa Kenya wanatarajia kuweka historia kwa mara ya kwanza kwa kurusha satelaiti waliyotengeneza nchini humo inayotumwa katika sayari nyingine kwa lengo la kukusanya taarifa za mabadiliko na utabiri wa hali ya hewa, ufuatiliaji wa wanyamapori ufuatiliaji wa ukanda wa habari na usafirishaji ugavi.
Satelaiti hiyo imetengenezwa na wanafunzi na watafiti wa chuo Kikuu cha Nairobi kwa Ushirikiano na Shirika la teknolojia za sayari la Japan Space Agency ( JAXA).
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Peter Mbithi amesema mafanikio hayo ni dhihirisho ya hatua zilizopigwa nchini kuhusu utafiti wa teknolojia ambao unaweza kuchangia katika maendeleo yatakayokuza uchumi wa taifa.
-
Ethiopia na Kenya zaunda mkakati wa kupambana na ugaidi
-
Masauni: Sio utaratibu Jeshi la Polisi kupiga raia, chukua hatua za kisheria
Satelaiti hiyo yenye ukubwa wa sentimita kumi, iliyogharimu takribani dola za kimarekani milioni 1 itarushwa kwenye sayari kutoka kituo kilichopo japan na Waziri wa Elimu, Bi Amina Mohamed.
”Kutakuwa na tukio Japan katika sayari na hapa chuoni kile kitakachofanyika Japan kitashuhudiwa na baadhi ya wakenya ambao watakuwa huko” amesema Professa Mbithi.
Mkuu wa taasisi ya mafunzo ya uhandisi katika chuo hiko amesema satelaiti hiyo yenye uzani wa kilo 14 itasafirishwa hadi kwenye sayari mwendo wa saa saba mchana siku ya ijumaa.
Ameongezea kuwa huu ni mwanzo wa Kenya kushiriki kwenye sayansi ya sayari, ni mara yetu ya kwanza kupiga hatua hii lakini tunaamini ni uhimu katika ustawishaji wa sayansi nchini”.