Kenya imepunguza idadi ya wageni watakaoruhusiwa kuhudhuria harusi hadi kufikia watu 50 pekee, kutokana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona nchini humo.

Baraza linalojumuisha dini mbali mbali nchini humo limesema kuwa chakula kinachotolewa katika harusi kitakuwa kikitilewa kwa ajili ya wazazi na ndugu wa damu wa maharusi pekee.

Mwezi Agosti Rais Uhuru Kenyatta aliongeza idadi ya wageni wanaoweza kuhudhuria harusi hadi watu 100 alipolegeza masharti ya kudhibiti maambukizi ya Covid-19.

Katika masharti mapya yaliyotangazwa Alhamisi wiki hii, chakula kimepigwa marufuku katika mazishi na idadi ya watu wanaoruhusiwa kuhudhuria mazishi, imepunguzwa hadi watu 100 pekee.

Masharti mengine ni kwamba huduma za kanisa sasa hazitatolewa kwa zaidi ya dakika 90, na muda wa mazishi pia umerekebishwa kwa kupunguzwa hadi saa moja pekee.

Wiki iliyopita mwenyekiti wa baraza la dini mbali mbali nchini Kenya, Anthony Muheria, alitibiwa virusi vya corona katika hospitali moja mjini Nairobi.

Simba SC kutinga Jos, balozi Bana aipa baraka
Azam FC yataja sababu ya kusitisha mkataba

Comments

comments