Mahakam Kuu ya nchini Kenya imetambua utoaji mimba kuwa ni Haki ya Msingi inayotambuliwa na Katiba ya Kenya
Mahakama hiyo imesema kuwakamata wanaotoa mimba ni kinyume cha Sheria kwa kuwa anaetoa kwa kufuata sheria na taratibu za kiafya ni ruhusa.
Polisi nchini humo wamekuwa wakiwakamata watumishi wa Afya na Wanawake kwa tuhuma za utoaji mimba.
Mapinduzi ya sheria hiyo yametokana na kesi ya hivi karibuni ya binti wa miaka 16 ambaye alikua mjamzito na baadae kutafuta ushauri wa kitaalamu na kusaidiwa kutoa ujauzito ambao mtoto alikua tayari amefariki.
Binti huyo alikamatwa Novemba mwaka jana na kujikuta akitakiwa kuhukumiwa kwa sababu ya utoaji mimba na baadae kesi iliposikilizwa ikagundulika hapakuwa na njia nyingine ya kitaalam ili kuzuia utoaji mimba huo usifanyike
Kituo cha Afrika cha Afya ya Uzazi kimesema maamuzi ya mahakama ni ushindi kwa watumishi wa afya na wanawake waliokuwa wanahitaji huduma hiyo.