Kampuni ya usafiri ya Roam Kenya-Swedish yenye makao yake makuu jijini Nairobi imezindua basi la umeme ambalo linatajwa kuwa rafiki wa mazingira kwa kutotoa moshi kama ilivyo kwa magari mengine yanayotumia nishati ya mafuta.

Mratibu wa mradi wa Roam nchini Kenya, Dennis Wakaba amesema “Hii inawakilisha mabadiliko kuelekea usafiri bora wa umma, tunaweza kuwa na watu wapanda kwa starehe na kufurahia safari kwa dhamiri safi, kwa sababu tunazungumza kuhusu utoaji wa hewa sifuri.”

Basi hilo, ambalo ni la kwanza la usafiri wa umma nchini Kenya lilifaniwa ubunifu tangu mwaka jana (2021), na lilitengenezwa kwa ushirikiano na mshirika wa kimataifa.

Hata hivyo, usafiri mwingi wa abiria unaendeshwa kibinafsi jijini Nairobi na Roam alisema nauli za basi la umeme zingeshindana na zile zinazotolewa na washindani wake wa moshi.

Aidha, bado kutakuwa na changamoto ya uwepo wa kituo kimoja cha kuchajia kilichopo katika jiji kuu la Nairobi, huku, timu ya Roam ikisema haitakatishwa tamaa na kwamba watahakikisha wanayafikia malengo waliyoyakusudia ili kupunguza magari yanayotoa moshi unaoathiri mazingira.

Ukali wa maisha: Waziri Mkuu atangaza kujiuzulu
Marekani yajipanga tishio la kuvamiwa na Taiwan