Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesimamisha shughuli zote za kimichezo nchini humo kwa muda usiojulikana hii ikiwa ni katika juhudi za kukabilina na wimbi la tatu la mlipuko wa virusi vya Corona nchini humo.

Jana Ijumaa Rais Kenyatta alitangaza kuzifunga kaunti tano za Nairobi, Kajiado, Machakos, Kiambu na Nakuru nchini humo kufuatia ongezeko la wagonjwa wa corona.

Marufuku hiyo imeanza saa 6 ya usiku wa leo ambapo hakutakuwa na usafiri wa barabarani, angani na reli utakaoruhusiwa kuingia na kuondoka katika sehemu hizo zilizotajwa kama zenye janga ‘kubwa la corona’.

Maeneo hayo yatakuwa chini ya masharti hayo ya zuio kwa siku 30 zijazo .

NEC yatangaza Uchaguzi mdogo Muhambwe
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Machi 27, 2021