Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametofautina mtazamo kuhusu ushoga na ndoa za jinsia moja na mgeni wake ambaye ni Rais wa Marekani, Barack Obama mbele ya waandishi wa habari.

Akiongea mbele ya idadi kubwa ya waandishi wa habari katika eneo la Ikulu ya Kenya, Rais Obama alipinga kwa nguvu ubaguzi dhidi ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, lakini Uhuru Kenyatta alikuwa ngangari na kumueleza kuwa utamaduni huo hauna nafasi nchini Kenya.

Rais Kenyatta alifafanua kuwa suala la ushoga sio suala muhimu nchini humo na kwamba nchi hiyo inahitaji kujikita katika maeneo mengine ambayo ndiyo maisha ya kila siku ya wananchi.

Obama aliingia nchini Kenya Julai 24 usiku na kupata mapokezi ya kihistoria katika nchi hiyo inayomchukulia kama mtoto wa nyumbani aliyerudi na taji la ukuu wa nchi kubwa yenye nguvu zaidi duniani.

AS Monaco Wakubali Yaishe Kwa Moutinho
Ubahili Wa Arsene Wenger ‘Kwishaaaaa…’