Rais Uhuru Kenyatta amewashauri Wakenya kuwachagua viongozi walio na uwezo wa kuliunganisha taifa linapoelekea katika uchaguzi mkuu.

Rais Kenyatta alikuwa akizungumza Ikulu ambako alikutana na viongozi wa dini ya Kiislamu kutoka pande zote za nchi kwa ajili ya Iftar.

Kenyatta aliendelea kumpigia debe kinara wa ODM Raila Odinga akisema kuwa Wakenya wanapaswa kumchagua kiongozi ambaye ataleta suluhisho kwa matatizo yanayowakabili wananchi.

Rais Uhuru Kenyatta akihutubia waalikwa wa Iftar Ikulu

“Sasa iwapo unaangalia mtu wa kulaumu badala ya kusuluhisha, wewe utakuwaje mtu mwenye suluhisho? Wewe ni mtu wa kuangalia tu shida. Na nchi hii inataka mtu wa kusuluhisha matatizo kwa sababu hakuna siku itakamilika bila matatizo. Shida zitakuwepo kila siku, Kuongoza Taifa si Rahisi Vile Unafikiria,” alisema Kenyatta.

Rais Kenyatta ameendelea kusema Raila akisema kuwa yeye ndiye kiongozi bora wa kuchukua usukani wa taifa baada ya uchaguzi wa Agosti kwa kuwa ni kiongozi komavu na mkweli anayeipenda nchi yake kutoka moyoni na mwenye rekodi ya kupigania taifa.

“Ninawaomba nyote muungano chini ya Mrengo wa Azimio. Nikiangalia kushoto au kulia, sioni mtu mwengine aliye na uwezo wa kutuunganisha. Sioni mwengine aliye na uwezo wa kusamehe au kuwa mtulivu kuliko Raila,” Rais Kenyatta alisema.

Kenyatta amewataka Wakenya kuendelea kuiombea nchini yao wanapojiandaa kuchagua viongozi ambao watajituma kusuluhisha matatizo yanayowakumba Wakenya.

Fahamu nchi za Kiislamu zinazozuia ndoa za Mitala
Yaliyomkuta R Kelly yamgeukia Trey Songz