Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametuma ujumbe na salamu za rambirambi kwa familia na ndugu wa wanafunzi 14 wa Shule ya Msingi Kakamega waliofariki dunia kwa kukanyagana kwenye ngazi, baada ya kengele ya kuwaruhusu kwenda makwao.

Kupitia ujumbe huo alioutoa Jumatatu jioni, Februari 3, 20120, Rais Kenyatta aliwaombea faraja wafiwa, majeruhi wapone haraka na kueleza kuagiza uchunguzi wa kina kufanyika kwa haraka.

Jumatatu iliripotiwa kuwa watoto 13 walikuwa wamefariki, lakini hadi kufikia jioni idadi hiyo iliongezeka baada ya mtoto mmoja aliyekuwa anapatiwa matibabu naye kupoteza maisha.

Kwa mujibu wa Citizen TV, watoto wawili waliojeruhiwa kwenye tukio hilo wanapatiwa matibabu kwenye Chumba cha Uangalizi Maalum (ICU) katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Kakamega.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi, wanafunzi wengi waliofariki dunia walikuwa Darasa la Tano, wakiwa wanaondoka madarasani kuelekea nyumbani majira ya saa kumi na moja jioni.

Ripoti za awali zinaeleza kuwa walimu walikuwa wanawachapa baadhi ya wanafunzi, hali iliyosababisha baadhi yao kukimbia kuelekea kwenye msongamano wa wanafunzi wengine hali iliyosababisha baadhi kuanguka, kubanwa na kukanyangwa.

Magufuli amkumbuka Moi kwa kufufua Jumuiya ya Afrika Mashariki
Micho akabidhiwa fupa lililomshinda kocha wa Simba Sven Vandenbroeck