Mahakama kuu ya Shanzu nchini Kenya, imemuachilia huru Pastor Ezekiel Odero kwa dhamana ya shilingi milioni 1.5, akisubiri kukamilika kwa uchunguzi kuhusu madai ya vifo kanisani mwake.
Mahakama kuu hiyo pia iliorodhesha ombi lililowasilishwa na Mhubiri Ezekiel Odero kama la dharura, baada ya Odero kuitaka Mahakama itoe agizo la kuizuia Serikali isifunge akaunti zake 15 za benki.
Mhubiri, Ezekiel Odero akiwa nje ya Mahakama kabla ya kuachiliwa kwa dhamana.
Mhubiri huyo wa Kanisa la New Life International lililopo Mavueni Kaunti ya Kilifi, Pwani ya Mombasa alifikishwa Mahakamani hapo hii leo (Mei 4, 2023), baada ya kuwa ndani tangu kukamatwa kwake wiki moja iliyopita.
Awali, upande wa Mashitaka uliiomba Mahakama indelee kumshikilia Mchungaji huyo kwa siku 30 zaidi, ukidai unaendela kukamilisha upelelezi dhidi ya mtuhumiwa na kwamba uwepo wake nje unaweza kuharibu ushahidi.