Jaji John Bates wa nchini Marekani, ameitupilia mbali kesi dhidi ya Mwanamfalme wa Saudi Arabia, Mohammed Bin Salman kuhusiana na mauaji ya mwaka wa 2018 ya mwandishi habari, Jamal Khashoggi.
Kufuatia hukumu hiyo, Jaji Bates ameonesha wasiwasi kuhusiana na uamuzi wake lakini akasema ilimbidi kufuata pendekezo la karibuni la Wizara ya Sheria ya Marekani, kuwa Bin Salman apewe kinga ya kushitakiwa.
Aidha, wasiwasi wa Bates unatokana sio unatokana na tuhuma za kuaminika za kuhusika kwa mwanamfalme huyo katika mauaji ya Khashoggi, lakini pia na uteuzi wa bin Salman kuwa Waziri Mkuu wa Saudi Arabia.
Kesi hiyo. iliwasilishwa na mchumba wa Khashoggi, Hatice Cengiz, ambaye anamtuhumu Rais wa Marekani, Joe Biden kumpa kinga Mwana mfalme Mohammed Bin Salman.